Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto)
akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty
linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es
Salaam jana.
Wateja wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige leo amezindua
rasmi rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa
jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika
barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua
duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni
mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna
Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza
kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla
ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa
umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa
wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa
nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.
Mmiliki wa duka la urembo la
ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke
Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa zake za urembo
ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa Mbunge wa
Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia
bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty
lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana
Diaspora Jestina George Meru.
Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.Wateja wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Michuzi Media Group ikiongozwa Ahmad Michuzi mwanalibeneke wa Michuzijr Blog ( wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwanalibeneke wa Fullshwangwe Blog John Bukuku wakiwasili kwenye uzinduzi huo.
Aidha
alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na
mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia
natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa
sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati
huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona
fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa
wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja
likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza
kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi
hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto
hii”.
Post a Comment