Nyota wa muziki wa Bongo Flava hapa nchini Diamondplatnumz amemjibu mchekeshaji Eric Omondi
kufuatia tukio lililotokea katika tamasha la Raha Fest lililofanyika nchini Kenya baada ya msanii Willy Paul kupanda kinguvu stejini muda ambao Diamond alitakiwa kuperfom huku akidai kuwa wasanii wa
Kenya wanadharauliwa nyumbani kwao.
Baada ya tukio hilo lililopelekea Diamond kushindwa ku-perfom katika tamasha hilo mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya aliweka chapisho katika mtandao wake wa Instagram akielezea namna ambavyo wasanii wa Kenya wamekuwa wakichukuliwa poa huku wasanii kutoka Tanzania wakipewa ‘treatment’ nzuri tofauti na wazawa.
Baada ya chapisho hilo Diamond aliachia ujumbe kwenye uwanja wa comment wa chapisho hilo ambapo alimtaka Omondi kuacha kuhamasisha chuki badala yake kuwasihi wasanii wa Kenya waongeze juhudi katika muziki wao.
“My brother Eric mafanikio hayaji kwa kuwawekea chuki wengine bali yanakuja kwa kuongeza juhudi kisha Mungu naye atakubariki...”
Tukio hilo limeibua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii, huku kila moja akiongea lake.
Post a Comment