Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Barabara za Kilomita 10 za Micheweni - Kiuyu-Maziwa Ng'ombe na Barabara ya Michweni -Shumba Mjini hadi Bandarini Wilaya ya Micheweni , Mkoa wa Kaskazini Pemba.
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amewahakikishia Wananchi wa Pemba kuwa Barabara nyingi Kisiwani humo
zitajengwa kwa Kiwango cha Lami.
Rais Dk Mwinyi ameyasema hayo alipozindua
Barabara za Kilomita 10 za Micheweni - Kiuyu-Maziwa Ng'ombe na Barabara
ya Michweni -Shumba Mjini hadi Bandarini Wilaya ya Micheweni , Mkoa wa Kaskazini
Pemba.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali ina
Programu Maalum ya Kuziwekea Taa Barabara zote zilizojengwa kwa Kiwango cha
Lami nchi nzima.
Rais Dk.Mwinyi amewahimiza
Wananchi kuacha kujenga katika
Hifadhi za Barabara kwani zimetengwa maalum kwa ajili ya kuendeleza
Miundombinu mengine.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa
kumekuwa na tabia ya watu kujenga
Pembezoni mwa Barabara kwa kutegemea kulipwa Fidia na Serikali jambo ambalo sio
sahihi.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amezitaka Halmashauri Kusimamia suala
hilo na kudhibiti Utoaji wa vibali
holela vya Ujenzi Pembezoni mwa Barabara.
Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu ya Ujenzi wa Barabara Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Dk, Habiba Hassan amesema Ujenzi wa Barabara hizo zenye Urefu wa Kilomita 10 ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya
2020-2025 ,Dira ya Maendeleo ya Zanzibar, Mpango Mkuu wa Maendeleo wa Taifa na
Mpango Mkuu wa Usafiri ambapo Barabara zenye Urefu wa Kilomita 140.9 zimejengwa Unguja na
Kilomita 134.9 zimejengwa Pemba.
Hafla ya uzinduzi wa barabara hizo ikifanyika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia ) akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa Barabara hizo.
Post a Comment