......................................
Na Mwandishi Wetu, Kibondo
SERIKALI ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imesema Sh bilioni 46.4 zilizotolewa na serikali zimetekeleza miradi mikubwa ya kijamii na kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi wilayani humo ikiwemo ongezeko kubwa la mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kibondo, Kanali Agrey Magwaza amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kigoma iliyofanya ziara kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.
Kanali Magwaza amesema kiasi hicho cha pesa ni sehemu ya Sh trilioni 11.5 zilizotolewa na serikali kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati mkoani Kigoma ambapo kwa Kibondo imeifungua wilaya hiyo kiuchumi lakini kuimarisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Diocles Rutemwa amesema kupitia fedha hizo halmashauri imetekeleza miradi ambayo imesaidia kuongeza mapato ya ndani ambapo kwa sasa halmashauri inaweza kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 3.
Post a Comment