MaMa Samia legal Aid Campaign yawafikia Wananchi wa Arusha

 

                         

                          NaPamela Mollel, Arusha 

Kampeni ya msaada wa kisheria wa MaMa Samia Legal Aid campaign inayotekelezwa na Wizara ya katiba na sheria imefanikiwa kutatua migogoro 136 kati ya migogoro 677 waliyoipokea.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa huduma za msaada wa kisheria kutoka wizara hiyo Ester Msambazi amesema mafanikio hayo wameyapata toka waanze kampeni hiyo March 1,2025 ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani ambapo inafanyika kitaifa jijini Arusha 

Ameongeza kuwa hadi kufikia Machi 7,wameweza kufikia wananchi 1844 huku idadi kubwa ikiwa ni wanaume wamejitokeza zaidi ukilinganisha na wanawake ambapo pia wameweza kupokea migogoro 677

"Kwenye migogoro zaidi wamejitokeza wanaume na tumeweza kuwaandikia makubaliano"Anasema Msambazi

Aidha aliongeza kuwa kuwa migogoro ilioongoza ni ya ardhi huku mkoa wa Arusha ukiwa unaongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya madai.

Kwa upande wao baadhi ya wanachi walionufaika na maaada wa kisheria walipongeza hatua hiyo kwa kuwa imekuja kutenda haki bila upendeleo

Post a Comment

Previous Post Next Post