Na Zuhura
Jafari, Mbeya
MBUNGE wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson amewataka Wana CCM Mkoa wa Mbeya kuendelea kuwa wamoja na kukijenga chama hicho.
Dkt. Ackson
ameyasema hayo Machi 2, 2025 wakati alipokuwa akizungumza na wana CCM wa Kata ya
Nonde jijini humo alipofanya ziara ya siku moja ya kuwatembelea kwa lengo za
kujua kero walizonazo ili kuzitafutia ufumbuzi.
“Nawaombeni
tuendelee kupendana na kushikimana hasa katika kipindi hiki tunachoelekea
kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu,” alisema Dkt. Tulia.
Aliwaomba
wana CCM hao wakati wa uchaguzi mkuu utakapo wadia wajitokeze kwa wingi kupiga
kura na kuhakikisha wanampa kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Dkt.
Tulia aliwataka wana chama hao kuacha kuanzisha makundi ambayo yataweza
kuwagawa wanachama jambo ambalo sio zuri kwani malengo yao ni kuhakikisha
wagombea wote wa CCM wanapata ushindi mnono kuanzia, diwani, mbunge na Rais.
Post a Comment