Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo tarehe 19.03.2025 yakutana na uongozi wa Tanzania Bloggers Netwark (TBN) katika ofisi za TCRA makao makuu Jijini Dar Es Salaam.
Katika kikao hicho TBN imeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa blogs kama sio kuziondoa kabisa.
Pia TBN imeiomba TCRA iwe inatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa bloggers ili kuwapa uzoefu.
TCRA wamesema kuwa wameyapokea maombi ya TBN na watayafanyia kazi.
"Tunafurahi kukutana nanyi leo, na kujadiliana haya maana Bloggers mna umuhimu mkubwa sana kwenye maudhui ya ndani. Na waahidi tumepokea maombi yenu, tutayanyia kazi na majibu tutawapatia"
Alisema Maneja wa Huduma za Utangazaji Eng Andrew Kisaka.
Post a Comment