Hatua hiyo ya kukusanya maoni imekuja kufuatia wataalamu hao kuagizwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ipo katika utafiti maalum kwa nia ya dhati kuboresha Sera na kanuni zake mbalimbali katika eneo
hilo la majukwaa ya mtandaoni.
Kikao hicho kimefanyika kwa mafanikio katika ofisi za TBN zilizopo kwa Aziz Ali, Temeke, watafiti hao wamechukua maoni ya TBN Makao Makuu, wakisema pia watafika katika Ofisi za Kanda za TBN.
Hali hiyo imefanya idadi kubwa ya wana TBN kushindwa kumudu kuendesha mitandao yao, Mwanzo TBN ilikua na wanaachams 300+ waliokuwa wamesajiliwa na TNB, lakini walipungua hadi kufikia 100+ wanaoweza kulipia japo wengine ni kwa kusuasua!"
Ameshauri pia TCRA kuendelea utamaduni wa kukutana na wadau wake ikiwamo na kuwapa mafunzo ya kuwaimarisha uwezo wao pamoja na kuangazia athari za gharama za bando za mtandao na vifaa.
Amesema ikiwa sekta ya blogging ndani ya tasnia ya habari ikisimamiwa vizuri kwa ushirikiano wa karibu na TCRA ni wazi kwamba Tanzania itanufaika na maudhui bora na yenye viwango ambayo yatasaidia kulinda maadili ya jamii yetu.
Post a Comment