WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE KANDA YA KUSINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Coletah Kokutangilila (kushoto) na Simon Mollel,  watumimishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipotembelea banda la maonesho la NIDA kabla ya  kufungua Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi, Machi 6, 2025. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju  na wa tatu kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack.  (Picha na Ofisi ya Waziri MNkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mchapisho mbalimbali  alipotembelea banda la maonesho la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kufungua  Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoa wa Lindi, Machi 6, 2025.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na wengine kutoka kushoto ni Watumishi wa TAKUKURU, Theodora Paschal, Emma Mwasyege na Deborah Nkwabi.  (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Stella Andrea kutoka Taasisi ya  Utafiti wa Kilimo   Tanzania (TARI) Naliendele  ambaye alitoa  maelezo kuhusu miche ya zao la korosho wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la maonesho la TARI  kabla ya kufungua Kongamano la Wananwake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye Uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoani Lindi, Machi 6, 2025. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea na baadae  alifungua  Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye uwanja wa Maegesho,  Nachingwea mkoani Lindi, Machi 6, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua   Kongamano la Wanawake Kanda ya Kusini lililofanyika kwenye uwanja wa Maegesho, Nachingwea Mkoani Lindi, Machi 6, 2025.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)







 

Post a Comment

Previous Post Next Post