WATU NANE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 31 KUJERUHIWA KUTOKANA NA AJALI MWANGA



               Na Ashrack Miraji Fullshagwe Media 

WATU nane wamefariki Dunia na wengine thelathini na moja kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Jeremiah Mkomagi alisema kuwa, tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi katika barabara ya Ugweno – Mwanga. 

Alisema kuwa, basi kampuni ya Mvungi lililokuwa likitokea Vuchama Ugweno kuelekea jiji Dar es salaam lilipokuwa likilikwepa gari dogo ndipo lilienda pembezoni mwa ngema ya mlima ambapo uzito uliizidi ngema na kupelekea kuanguka bondeni.

“Kama unavojua kipindi hiki ni cha mvua sasa dereva wa hili basi alikuwa analikwepa gari dogo akawa ameenda pembeni ya kingo ya mlima ndipo uzito ulipolea na kupelea kuangukia bondeni” Alisema Mkomagi. 

Alisema kuwa, watu saba walifariki Dunia pale pale huku mmoja akifariki wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Kanda ya KCMC na wengine 31 kujeruhiwa ambapo majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kifula pamoja na Hospitali ya Kanda KCMC. 

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa hospitali ya Kanda ya KCMC, Gabriell Chiseo amethibitisha hospitali hiyo kupokea majeruhi saba ambapo wa kike ni wanne na wakiume watatu. 

Chiseo alisema kuwa, kati ya majeruhi hao mmoja alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu ambaye ni mwanamke

Post a Comment

Previous Post Next Post